Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 29, 2017

MALI YATETEA UBINGWA WAKE WA AFCON U-17 Historic as Mali retain cadet crown
MALI imefanikiwa kutetea taji lake la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 baada ya kuifunga Ghana bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika jana usiku.
Timu hiyo ambayo nusura isishiriki mashindano hayo kutokana tishio la kutaka kufungiwa na Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) miezi michache iliyopita, ilidhihirisha ubora wake kwa kuwafunika wapinzani wao hao wa Ghana.
Mamadou Samake ndiye aliyefunga bao hilo pekee katika mchezo huo katika dakika ya 22 katika mchezo uliojaa msisimko na kushuhudia Mali ikiungana na mataifa makubwa katika soka ya Ghana, Nigeria na Gambia kutwaa taji hilo mara mbili.
Hata hivyo, Mali ni nchi ya kwanza kutetea taji hilo.
Black Starlets walishindwa kuonesha kiwango chao cha awali, ambacho kiliwafanya kufunga mabao tisa katika mechi mbili za kwanza katika mashindano hayo.
Timu hiyo ilishindwa kabisa kufanya mashambulizi ya nguvu langoni mwa wapinzani wao.
Ghana walikosa penalti mbili katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo, ambazo ziliokolewa na kipa wa Mali, Ibrahim Danlad.
Beki ya Ghana ilishindwa ilishindwa kufanya maamuzi ya haraka kumzuia Danlad aliyetoa pasi kwa Samake ambaye kwa haraka alifunga bao hilo.
John Otu na Razak Yusif waliadhibiwa kwa mchezo mbaya adhabu zilizoshuhudia Ghana wakipewa penalti na kushindwa kufunga.
Gabriel Leveh alikaribi kuwasawazishia Starlets mwishoni mwa kipindi cha kwanza, lakini kipa Youssouf Koita alidokoa mpira huo uliokuwa ukielekea langoni.
Mali katika mchezo wa kwanza wa Kundi B ililazimishwa sare ya bila kufungana na timu ya taifa ya Tanzania, Serengeti Boys, ambayo ilikuwa ikishiriki kwa mara ya kwanza mashindano hayo.
Timu zote za Ghana na Mali pamoja na Guinea, iliyoifunga Niger na kumaliza ya tatu, zitaiwakilisha Afrika katika fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini India Oktoba.