Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 29, 2017

Griezmann kubaki Atletico MadridImage result for Griezmann
MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amepuuza taarifa kwamba tayari amekubali kuondoka kwenye klabu yake wakati huu wa majira ya kiangazi.
Griezmann amehusishwa na kujiunga na Manchester United majira ya kiangazi na uwezekano huo ukichagizwa na klabu hiyo ya England kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya kupitia ubingwa wa Europa baada ya kuifunga Ajax mabao 2-0 kwenye fainali.
Taarifa mbalimbali zinasema makubaliano binafsi yamefikiwa kati ya mshambuliaji huyo na Manchester United, huku ikitazamiwa atasaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo haraka.
Mshambuliaji aliongeza uvumi wa kujiunga na klabu hiyo ya England pale aliposema nafasi ya yeye kuelekea Manchester United ina uwiano wa sita kwa 10.
Hata hivyo mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alitumia akaunti yake ya Twitter Ijumaa hii kukanusha taarifa hizo, ingawa alikiri kuwa hatima yake bado haieleweki.
“Uvumi wote hauna msingi,” aliandika na kuongeza kuwa: “Bado niko Atletico Madrid. Muelekeo wangu utajulikana baada ya mazungumzo na mshauri wangu wa michezo.”
Mapema juzi alisisitiza kuwa anataka kushinda mataji chini ya kocha Diego Simeone.
“Umekuwa mwaka mzuri na nina imani naweza kuwa bora zaidi na kushinda mataji na timu hii,” alisema Griezmann na kuongeza kuwa:
 “Nitafanya kila kinachowezekana. Tuna furaha sana hapa. Tumefikia malengo yetu, labda tulihitaji zaidi, lakini haikuwezekana.”