Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 29, 2017

MKUDE AINGIA KAMBINI TAIFA STARS BAADA YA KUTOKA HOSPITALI LEO



 
NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude ameruhusiwa kutoka hospitali alipokuwa amelazwa tangu juzi baada ya kupata ajali ya gari eneo la Dumila mkoani Morogoro na ameshajiunga na kikosi cha Taifa Stars
Mkude alikuwa amelazwa hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili, Dar es Salaam kufuatia ajali baada ya gari walilikuwa wakisafiria kupasuka gurudumu moja na kupinduka na kusababisha kifo cha Shose Fidelis.
Akizungumza na gazeti hili Mkude alisema yuko vizuri na hana tatizo lolote ukiondoa michubuko kidogo aliyopata.
“Daktari amesema nilipata mshituko tu baada ya ajali, lakini sijaumia popote na ninaweza kuendelea na kazi zangu kama kawaida,” alisema   Mkude.
Kabla ya kuhamishiwa Muhimbili Mkude pamoja na majeruhi wengine walipata huduma ya kwanza katika kituo cha afya Dumila na baadae kuhamishiwa hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Mkude alikuwa anatoka Dodoma, ambako Jumamosi aliisaidia Simba kukata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Watu wengine wawili waliokuwa katika gari hili Jasmin na Faudhia wamelazwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro na dereva ambaye pia ndiye mmiliki wa gari ajulikanaye kwa jina la utani, Rais wa Kibamba anashikiliwa na Polisi.
Hii ni ajali ya tatu kwa Mkude,  alipata ajali Mbezi Dar es Salaam lakini hakupata majeraha ya pili na ya tatu ni wakati anapelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi gari yao ikamgonga mwendesha boda boda napo hakupata majeraha.

No comments:

Post a Comment