LONDO,
England
ARSENAL
imeweka ofa nyingine mezani kumbakisha nyota wake Alexis Sanchez anayesakwa na
Bayern Munich.
Mkataba
huo unafahamika ni wa mshahara wa pauni 270,000 kwa wiki, ambao ni kidogo
kulinganisha na kiasi cha pauni 300,000 kwa wiki anachotaka mshambuliaji huyo
wa kimataifa wa Chile, ingawa ofa hiyo ina marupurupu mengi ambayo inakaribia
kufikia pauni 300, 000 wanazotaka.
Bayern
inatajwa kumuwania Sanchez kama atakataa kusaini mkataba mpya na Arsenal,
wakati huu wa majira ya kiangazi, lakini pia klabu za Juventus na Paris
Saint-Germain zinamuwania mshambuliaji huyo.
Uvumi
ulizagaa wiki hii kuwa ameshafanya uamuzi baada ya Chama cha Soka cha Chile
kumuorodhesha kwa bahati mbaya kwenye kikosi cha timu yao kuwa mshambuliaji
huyo anatokea Bayern Munich.
Alex
Oxlade-Chamberlain pia anatarajia kuanza mazungumzo ya mkataba mpya baada ya
fainali za Kombe la FA. Chamberlain yuko mwaka wa mwisho wa mkataba wake na
Liverpool inatajwa kumuwania winga huyo.
No comments:
Post a Comment