Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 29, 2017

Romero ataka awe wa kwanza Man UnitedImage result for SERGIO ROMERO
MANCHESTER, England
BAADA ya kuonesha umahiri golini, golikipa wa Manchester United, Sergio Romero anataka klabu hiyo imfanye awe chaguo la kwanza hapo.
Romero aliyechaguliwa na kufanya vyema kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Europa anamwambia kocha wake, Jose Mourimnho asiwe na shaka hata kama kipa namba moja, David de Gea ataondoka Old Trafford.
Ni katika msingi huohuo, Romero anataka kuona kwamba hasajiliwi kipa nyota kutoka nje kwa ajili ya kuwa chaguo la kwanza, bali apewe yeye, kisha madogo wachukue nafasi ya pili,tatu na nne na wana uhakika wa kufanya vizuri.
De Gea amecheza mechi 36 kati ya 38 za Ligi Kuu ya England, na kwa mara nyingne tena anawaniwa na Real Madrid wanaopenda kuvunja rekodi za usajili. Madrid ndio nyumbani kwa De Gea.
Msimu uliopita klabu mbili hizo zilikubaliana dakika za mwisho juu ya mauzo ya mchezaji huyo, lakini nukushi iliyotumwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ilichelewa kufika baada ya muda wa mwisho ambao ilikuwa ni saa sita usiku. Kwa sasa Mourinho anataka iwapo watamchukua, wawape AlvaroMorata.