Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 27, 2017

TAMASHA LA BODABODA LAJA


Meneja Mkuu wa kampuni ya JP Decaux Ltd, Bwana Shaban Makugaya (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu tamasha la bodabodaDar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa JP Decaux Ltd, Bwana Elias Richard.


KATIKA kukabiliana na ajali za pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam, Kampuni ya JP Decaux Tanzania wakishirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la International Republican Institute (IRI) wameandaa tamasha kwa ajili ya kutoa elimu kwa waendesha pikipiki.
Akizungumza na waandishi wa habari  jijini hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa JP Decaux, Shabani Makunganya alisema tamasha hilo maalumu kwa wadau wa pikipiki litakaloitwa ‘Dar Bodaboda Superstar’ litafanyika Mei 17 mwaka huu, Dar es Salaam.
Alisema lengo la tamasha hilo ni kuweka msisitizo na kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa pikipiki na abiria kwa dhumuni la kuzingatia sheria za usalama na matumizi ya barabara kwa ujumla sambamba na msisitizo wa kuwa na nidhamu ya kazi na juhudi ili kupata maendeleo.
“Tumeona kuna umuhimu wa waendesha pikipiki kupatiwa elimu juu ya usalama wao tayari tumeshatoa taarifa kwa jeshi la polisi usalama barabarani kwa ajili ya kushirikiana nao,”alisema Makunganya.
Alisema tamasha hili linatarajia kushirikisha waendesha pikipiki 5,000 kwa mkoa wa Dar es Salaam na baadaye watakwenda katika mikoa mingine, lengo ni elimu hiyo kufika kwa waendesha pikipiki wengi zaidi.
Aidha alisema wameamua kutoa elimu hiyo kwa waendesha pikipiki kwa kuwa usafiri huo umekuwa ni kati ya njia rahisi ya kumuwezesha msafiri kufika haraka hata pale inapotokea dharura.
“Licha ya manufaa ya usafiri huo ila ni wazi kuwa usafiri huo umekuwa unaongoza kwa kupata ajali zinazopelekea kupoteza maisha ya watu wengi sambamba na kuhusishwa na matukio ya uhalifu nchini, hivyo ni muhimu elimu hii kutolewa,”aliongeza.

No comments:

Post a Comment