Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 27, 2017

SANCHEZ HAUZWI KWA MPINZANI ENGLAND


Fowadi hatari wa Arsenal Alexis Sanchez hatauzwa kwa Mpinzani yeyote wa Arsenal huko England kwa mujibu wa Meneja wa Klabu hiyo Arsene Wenger.
Sanchez, Mchezaji wa Kimataifa kutoka Chile ambae Majuzi Jumapili aliifungia Arsenal Bao la ushindi walipowafunga Man City na kutinga Fainali ya FA CUP, amebakiza Mwaka mmoja tu kwenye Mkataba wake wa sasa huku akigomea kusaini Mkataba mpya.
Wenger ameeleza: "Sidhani kama unaweza kumuuza kwa Klabu nyingine ya Ligi Kuu England, huo ndio ukweli! Lakini kama nlivyosema nadhani atabaki na kusaini Mkataba!"
Ingawa yeye binafsi hajathibitisha kubaki Arsenal kwa Msimu ujao huku Mkataba wake ukiisha Juni, Wenger amesisitiza anashughulikia ununuaji Wachezaji wapya kwa ajili ya Msimu ujao. Ameeleza: "Nipo kazini hadi Siku ya mwisho ya Msimu nkishughulikia ya sasa na baadae. Ununuzi wa Wachezaji wapya hatima ya Klabu na ni muhimu. Hatima yangu si muhimu, ya klabu ndio muhimu"