Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 27, 2017

NGOMA, BOSOU KUIKOSA MBAO FC



Kikosi cha wachezaji 22 cha Yanga kimeondoka kwenda Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho (FA) nusu fainali dhidi ya Mbao FC utakaochezwa Jumapili ya wiki hii
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amewataja wachezaji wanaotarajiwa kuondoka ni makipa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Benno Kakolanya na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Oscar Joshua, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Hassan Kessy, Kevin Yondan, Andrew Vincent na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Viungo ni Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Said Juma ‘Makapu’, Juma Mahadhi, Simon Msuva, Geoffrey Mwashiuya, Obrey Chirwa na Emmanuel Martin wakati washambuliaji ni Amissi Tambwe na Matheo Antony.
Wachezaji wanne watakosekana beki Vincent Bossou, kiungo Yussuf Mhilu na washambuliaji Malimi Busungu na Donald Ngoma.
Bossou, Ngoma na Busungu ni majeruhi, wakati Mhilu yupo na kikosi cha timu ya vijana cha timu hiyo, ambacho jana kilitoa sare ya 1-1 na Kombaini ya timu ya Majeshi mjini Dodoma.  
Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la ASFC inatarajiwa kuchezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Azam FC na Simba SC.
Ikumbukwe Yanga SC ndiyo mabingwa watetezi wa Kombe la TFF baada ya kuifunga Azam 3-0 katika fainali mwaka jana.
Mara tu baada ya mchezo huo, Yanga inatarajiwa kurejea Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Prisons ya Mbeya.
Kocha Msaidizi Juma Mwambusi amesema kikosi chake kiko vizuri na tayari kwa mchezo huo wa Jumapili.
Alisema wanauchukulia kama fainali wakiamini ushindi utawawezesha kusonga mbele na kucheza fainali kwa mara ya pili baada ya kuchukuwa ubingwa msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment