Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 27, 2017

JESHI STARS YATETEA UBINGWA WA MASHINDANO YA WAVU YA MUUNGANO





TIMU ya  wavu ya Jeshi Stars imefanikiwa kutetea kombe la mashindano ya Muungano baada ya kuifunga Tanzania Prisons kwa seti 3-1  kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.
Jeshi Stars ambayo msimu uliopita ilicheza fainali na Mafunzo, nyota yake ilionekana kung’aa mapema kwani seti ya kwanza walimaliza kwa 25-13, seti ya pili 25-18, seti ya pili 22-25  na seti ya nne 25-15.
Jeshi Stars ilifuzu fainali baada ya kuifunga Chui kwa seti 3-1 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ambapo seti ya kwanza ilishinda kwa 25-21, 23-25, 25-22 na 25-18
Tanzania Prisons iliifunga Mafunzo kwa seti 3-0 ambapo seti ya kwanza ilishinda 25-21, seti ya pili 25-23 na seti ya tatu 25 -20.
Kwa upande wa wanawake Tanzania Prisons imeibuka bingwa baada ya kuizidi Jeshi Stars kwa kushinda seti nyingi kuliko Jeshi Stars lakini kila moja ikiwa na pointi tisa kwa sababu walicheza kwa mfumo wa ligi
Akizungumza na gazeti hili, Katibu Msaidizi wa TAVA, Alfred Selengia alisema mashindano yalikuwa na ushindani na idadi ya timu zimeongezeka tofauti na miaka ya nyuma na kufanikiwa kuchangua timu ya taifa ya wanawake na wanaume pia ya U-20.
“Mashindano yalikuwa na ushindani na wachezaji walionesha uwezo mkubwa na kupitia mashindano haya tumepata wachezaji 36 wa timu za Taifa za wanawake, wanaume nay a vijana ya U-20,” alisema Selengia
Pia Selengia alisema bingwa ndie atawakilisha nchi kwenye mashindano ya Afrika ambayo yatafanyika mwakani kwa timu za wanawake na wanaume
Timu zinazoshiriki ni bingwa mtetezi Jeshi Stars, Chui, Polisi Zanzibar, Moro Stars, Makongo sekondari, Tanzania Prisons, Saut Mwanza, Mafunzo ya Zanzibar, Dodoma, Mjimwema, Victory Sports na Kinyerezi.
Timu za wanawake ni Tanzania Prisons, Jeshi Stars, Shule ya Sekondari ya Makongo, Saut ya Mwanza, Mjimwema na Dodoma.

No comments:

Post a Comment