Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 27, 2017

HAFLA YA KUCHANGIA SERENGETI BOYS KESHO

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeandaa hafla maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya timu ya Taifa ya Vijana ‘Serengeti Boys’ inayojiandaa kucheza fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini Gabon.
Akizungumza na gazeti hili, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema hafla hiyo itafanyika Serena holeli kuanzia saa moja jioni kwa ajili ya kuchangisha pesa kwa ajili ya kuisaidia Serengeti boys inayoshiriki fainali za Afrika zitafanyika kuanzia Mei 14 -28, 2017.
 “TFF inatambua kuwa wadau mbalimbali wamekuwa wakichangia kupitia mitandao ya simu kama vile namba 0687 333 222 na Selcom kwa namba 22 33 44 pia kwenye akaunti Na. 00 866 280 03 katika Benki ya Diamond Trust (DTB),” alisema Lucas
Pia  lengo ni kukusanya shilingi bilioni moja na TFF imewakaribisha wawakilishi wa makundi mbalimbali ili wawasilishe michango yao na kumkabidhi mgeni rasmi. 
Kwa kutambua michango mbalimbali ambayo imekusanywa kupitia makundi ya mitandao ya jamii kama WhattsApp, facebook  TFF inaomba wawakilishi wa makundi yote ya mitandao ya jamii ambao wamekusanya michango hii wajiorodheshe ili wapate fursa ya kukabidhi michango ya makundi yao kwa mgeni rasmi katika hafla hii.
“Admins wanaombwa kujiorodhesha kwa kutuma email kwenda fdf@tff.or.tz, kwa kupiga simu 0787 176767 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda 0787 176767 ambayo pia inapatikana kwenye mawasiliano ya WhattsApp,” alisema Lucas
Pia Lucas alisema wawakilishi wa makundi mengine kama idara za Serikali, mashirika ya umma, ya binafsi na watu binafsi ambao wamechangia wanaombwa wajioredheshe ili wapewe fursa ya kukabidhi michango yao.
TFF inashukuru sana kwa ushirikiano, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Serengeti Boys