Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 3, 2017

SIMBA UWANJANI KESHO, YANGA WAO JUMAPILI

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea kesho na vinara wa ligi hiyo Simba inatarajiwa kuialika Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ukiacha mchezo huo, michezo mingine itakuwa ni kati ya Toto Africans na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza huku Kagera Sugar ikiikaribisha Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Azam FC pia itacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Chamazi. Mchezo huo utaanza saa 1.00 jioni wakati mechi nyingine zitaanza saa 10.00 jioni.

Jumapili Machi 5, mwaka huu Mtibwa Sugar itaialika Young Africans kwenye uwanja huo katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom utachezwa Uwanja wa Uhuru ambako African Lyon itaialika Mwadui ya Shinyanga wakati Ndanda FC itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona siku ya Jumatatu Machi 6, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment