Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 9, 2016

YANGA KUILIPA SIMBA MILIONI 50 SAKATA LA KESIYANGA imetozwa faini ya Sh milioni 3,000,000 na kutakiwa kulipa fidia ya Sh milioni 50 klabu ya Simba kwa kosa la kupeleka jina la mchezaji Hassan Ramadhani Kessy, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) huku akiwa ndani ya mkataba na klabu ya Simba.
Hukumu hiyo imetolewa leo na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji baada ya imebaini kuwa Juni 10, 2016 Yanga ilikiuka kanuni za ligi kifungu 69[5].
Akizungumza na gazeti hili, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Alfred Lucas alisema adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ili kila mwanachama wa TFF kulinda uadilifu wa soka la Tanzania.
“Mchezaji Hassan Kessy alikuwa na Mkataba na Simba uliokuwa unaishia  Juni 15, 2016 na Yanga walikiri mbele ya kamati kupeleka jina lake huko Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Juni 10, 2016 huku akiwa ndani ya mkataba na Simba,” alisema Lucas.
Pia Lucas alisema Yanga ilionesha mkataba uliosainiwa na Kessy Juni 20, 2016 jambo ambalo halikwa na sababu ya msingi ya kufanya mambo yaliyoainishwa kwenye kipengele cha 2 na cha 4 kabla ya kumalizika kwa mkataba kati Kessy na Simba.

 kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh 50,000,000 (Shilingi milioni hamsini).
Kamati imesema TFF kupitia Sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuielekeza Yanga hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Simba kama taratibu zinavyoelekeza mgogoro huu usingechukua sura ya sasa au usingekuwepo.
Katika sakata hili Simba walipeleka ushahidi wa machapisho yanayotokana na vyombo mbalimbali vya habari ukimwonyesha Kessy akiwa na viongozi wa Yanga.
Lucas alisema bila kuathiri hadhi ya uanachama wengine wa TFF, Simba ni brand kubwa kama ilivyo Yanga hivyo umakini unapaswa kutumika ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima.
Pia Kamati hiyo imemtaka Katibu Mkuu wa TFF kumchukulia hatua stahiki Ofisa wake aliyehusika ama kwa kushirikiana na uongozi wa Yanga kutuma jina la Kessy Caf.