Yanga imejikuta ikichezeshwa gwaride na wanajeshi wa
JKU baada kufungwa mabao 2-0 , katika mechi ya kujipima nguvu iliyochezwa
kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Hii ilikuwa mechi ya kwanza kwa kocha George
Lwandamina tangu achukue mikoba kwa Hans van Pluijm aliyepelekwa nafasi ya
Mkurugenzi wa Ufundi.
Mechi hiyo ni ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa
ligi unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 17 mwaka huu ambapo Lwandamina
aliitumia kuangalia kikosi chake.
JKU ilipata bao la kwanza katika dakika ya 11
likifungwa na Emmanuel Martin kwa shuti kali baada ya kuunganisha mpira wa kona
fupi kutoka kwa Feisal Salum.
Dakika ya 26 Martin aliifungia timu yake bao la pili
kwa shuti kali ndani ya box baada ya kumzunguka beki wa Yanga Pato Ngonyani.
Katika mechi hiyo ya jana, Lwandamina alitumia
vikosi viwili. Kikosi cha kwanza kilichokwenda mapumziko kikiwa nyuma kwa mabao
2-0 kilikuwa: Ally Mustafa 'Barthez', Hassan Kessy, Oscar Joshua, Pato
Ngonyani, Nadir Haroub 'Cannavaro', Said Juma, Juma Mahadhi, Matheo Antony,
Obrey Chirwa, Malimi Busungu na Geoffrey Mwashuiya.
Kikosi cha pili kilikuwa: Deogratius Munish, Juma
Abdul, Haji Mwinyi, Vincent Bossou, Andrew Vincent, Justine Zulu, Deus Kaseke,
Thaban Kamusoko, Donald Ngoma, Simon Msuva, Amis Tambwe na Deus Kaseke.
Hata hivyo kikosi hicho hakikubadi matokeo. Mchezaji
Zulu ambaye wengi walitaka kumuona alionyesha kiwango kizuri kwani alikaba na
kuchezesha timu ingawa ameonekana mzito.
No comments:
Post a Comment