Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 9, 2016

JONESIA AZAWADIWA GARI KWA KUCHEZESHA AFCON WANAWAKE
MWAMUZI wa soka wa kike wa Kimataifa, Jonesia Rukyaa, amezawadiwa gari aina ya Toyota Vitz na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) baada ya kufanikiwa kuchezesha kwa mafanikio fainali za Afrika za Wanawake.

Akizungumza wakati wa hafla ya kumpongeza, Jonesia, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema amefurahi kwa kiwango ambacho Jonesia amekionesha hadi kufanikiwa kuchezesha mchezo wa mshindi wa tatu kwenye faiinali hizo.

"Jonesia ameitangaza Tanzania kwa kiwango ambacho amekionesha, sasa kamati ya waamuzi mnatakiwa mfanye kazi ya kuwazalisha akina Jonesia wengi kutoka kwa wanaume na wanawake," alisema Malinzi

Pia Malinzi alisema ana imani Jonesia atachezesha fainali zijazo za Afrika na fainali zijazo za dunia kwani kwa sasa ni kati ya waamuzi bora watano barani Afrika kwa wanawake.
Malinzi alionesha kusikitishwa na waamuzi Martin Saanya na Samwel Mpenzu kuondolewa kwenye ratiba ya Ligi Kuu na kuitaka kamati kuchunguzza kwa makini na kutenda haki

Naye Jonesia Rukyaa aliwashukuru wadau wote wa soka kwa michsango yao mbalimbali ambayo wamekuwa wakimpatia kwani imemjenga na kumfanya kuwa bora na kutoa rai wanawake kuendelezwa kwnai wanaweza.

"Kiukweli sikutarajia kuchaguliwa kuchezesha fainali za wanawake barani Afrika kwani kwenye semina nilikutana na waamuzi wenye uzoefu zaidi ya miaka kumi huku mimi nikiwa na uzoefu wa miaka mitatu,|" alisema Jonesia

Pia aliishukuru TFF na Kamati ya waamuzi kwa kumpanga kuchezesha mechi za wanawake hasa za Simba na Yanga kwani zimemjenga na kumpa uzoefu.

Jonesia alichezesha mshindi wa tatu na kupewa medali ya dhahabu anasema walianza wakiwa waamuzi 11 lakini walimaza wakiwa nane tu kwa ilikuwa ukiharibu unaondolewa siku hiyohiyo.

Wakati huohuo, mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa timu ya soka la ufukweni dhidi ya Uganda unatarajiwa kuchezwwa leo badala ya kesho kwenye Uwanja wa Karume, Dar ees Salaam.