Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 3, 2016

VIONGOZI WA MATAWI SIMBA WAFANYA MKUTANO LEO 
Kwenye mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya klabu hiyo yaliyopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo na kuhudhuriwa na wanachama 200 kutoka matawi 68.
Awali akizungumza baada ya kufungua mkutano huo Rais wa Simba, Evans Aveva alisema mktano huo utajadili ajenda mbili ambazo ni mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania na mkutano mkuu wa dharura utakaofanyika Desemba 11.
“Ndugu viongozi wenzangu nimewaita hapa ili tujadili mkutano mkuu unaotarajia kufanyika Desemba 11 na mzunguko wa pili wa ligi kuu hivyo kabla ya kuanza kujadili naomba wandishi wa habari watupishe ili tuweze kuendelea na mkutano wetu,” alisema Aveva huku akishangiliwa kwa makofi.
Mkutano huo ambao ulianza saa tisa alasiri uliohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, Katibu Mkuu, Patrick Kahemele na wajumbe wa kamati ya Utendaji.
Awali Rais wa Simba, Evans Aveva alisema Kamati ya Utendaji imeitisha mkutano mkuu wa dharura unatarajiwa kufanyika Desemba 11, kwenye ukumbi wa Polisi Osyterbay Dar es Salaam.
Hata hivyo baraza la bodi ya wadhamini wa klabu hiyo chini ya Katibu wake Mkuu, Mzee Hamis Kilomoni juzi aliitisha mkutano wa wandishi wa habari na kudai mkutano huo ni batili na kumwomba mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuusimamisha.


VIONGOZI wa Matawi wa klabu ya Simba leo wamefanya mkutano na kujadili ajenda mbili kuu.