Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 2, 2016

MBAO FC YAPATA UDHAMINI MNONO LEO


 KLABU ya Mbao imepata udhamini wa 25 milioni kwa mkataba wa miezi sita huku wakipewa sharti moja kwamba wakifanya vizuri wataboreshewa mkataba huo.

Kampuni ya Hawaii Product Suppliers kupitia bidhaa yao ya Cowbell ndiyo wameipa jeuri Mbao FC ya jijini Mwanza ambayo ilikuwa na ukata mkubwa kwenye mechi za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ambapo wanashika nafasi ya 12 wakiwa wamekusanya pointi 16.

Menaja Masoko wa Kampuni hiyo, Elisaria Ndeta alisema kuwa wameamua kuingia mkataba na Mbao FC kutokana na kuvutiwa baada ya kufanya vizuri mechi za mwishoni kwenye mzunguko huo.

"Kama watafanya vizuri basi kuna maboresho kwenye mkataba wetu, tumedhamini baada ya kufurahishwa na kiwango chao kwenye mechi za mwisho mwisho mwa mzunguko wa kwanza, tunaamini watafanya vizuri zaidi," alisema Ndeta.          

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Mbao FC, Solly Zephania Njashi, aliishukuru kampuni hiyo kwa udhamini wa mechi 15 zilizobaki ambapo fedha hizo zitawasaidia kulipa mishahara wachezaji wao.

"Timu zenye matatizo ya fedha zipo nyingi, tunashukuru kwa udhamini huu ambao tunatakiwa kuutunza, sisi tutajipanga kuhakikisha tunafanya vizuri mechi zijazo ili tuendelee kunufaika na udhamini huu," alisema  Njashi.