Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 3, 2016

RIPHAT WA NDANDA AWA MCHEZAJI BORA WA NOVEMBAMCHEZAJI Riphat Hamisi wa Ndanda FC amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Novemba, msimu wa 2016/2017.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Afisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema Riphat ambaye ni mshambulaji aliwashinda wachezaji Shaban Idd wa Azam FC na Mbaraka Abeid wa Kagera Sugar.
“Riphat amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Novmba na atapata zawadi ya milioni moja toka kwa kampuni ya Vodacom ambao ndio wadhamini wa ligi kuu Tanzania Bara,” alisema Lucas
Katika mechi mbili ambazo timu ya Ndanda FC ilicheza kwa mwezi huo, Riphat aliisaidia timu yake kupata ushindi katika michezo yote, ambapo ilikusanya pointi 6 zilizoifanya kushika nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi
Pia aliifungia timu yake mabao mawili katika michezo miwili ambayo timu yake ilicheza kwa mwezi huo kwani ulikuwa na raundi mbili zilizochezwa.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Riphat atazawadiwa kitita cha Shilingi milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.