Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 3, 2016

AZAM FC NA SIMBA ZANUSA NUSU FAINALI LIGI YA VIJANA

TIMU mbili za kwanza kutoka kwenye kila kundi, Ligi ya vijana kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom zitafuzu hatua ya nusu fainali itakayoanza Desemba 9, Dar es Salaam.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema hatua ya nusu fainali itachezwa jijini Dar Es Salaam katika uwanja wa Azam Complex  kuanzia Desemba na fainali itachezwa Desemba 11,  katika uwanja huo huo.
“Ligi ya Vijana inatarajia kuendelea kesho kutwa (kesho) kwenye vituo vya Dar es Salaam na Kagera lakini pia timu mbili za juu kila kundui ndio zitakazofuzu hatua ya nusu fainali,” alisema Lucas. 
Katika kituo cha Dar es Salaam kesho, Simba inatarajiwa kucheza na JKT Ruvu mchezo utakaoanza saa 8.00 mchana na saa 10.30 kutakuwa na mchezo kati ya Tanzania Prisons na Ndanda FC ya Mtwara.
Leo katika kituo cha Kagera kutakuwa na mchezo kati Stand United itakayocheza na  Yanga saa 8.00 mchana wakati ya Mwadui itacheza na Mbao saa 10.30 jioni.
Jumatatu Kagera Sugar kucheza na African Lyon saa 8.00 mchana wakati Azam FC ya Dar es Salaam na Toto Africans zitacheza saa 10.30 jioni na kuhitimisha ratiba kwa kituo hicho.
Kituo cha Dar es Salaam, Majimaji itacheza na Ruvu Shooting  saa 8.00 mchana wakati Mtibwa Sugar ya Morogoro itacheza na Mbeya City saa 10.30 jioni.
Mpaka sasa kwa kituo cha Dar es Salaam Simba inaongoza na kituo cha Kagera Azam FC inaongoza.