Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 16, 2016

MBEYA SITY YASILIJILI WACHEZAJI 11 YAACHA SABA
KATIKA dirisha dogo la usajili lililofungwa jana usiku kiungo mkongwe wa Mbeya City, Ramadhan Chombo 'Redondo' ametupiwa virago pamoja na wenzake saba.

Wengine walioachwa ni Meshack Samwel, Peter Mwangosi, Michael Kerenge, Mackyada Franco, Issa Nelson, Salvatory Nkulula, Hemedy Murutabose wakati Joseph Mahundi ambaye alikuwa anahitajika kikosini humo alisaini Azam baada ya mkataba wake kumalizika.

Pia Mbeya City imetangaza nyota wapya 11 ambao ni Mrisho Ngassa, Juma Seif Kijiko, Hood Mayanja, Tito Okello, Zahor Pazzi, Hussein Salum, Otong William, Raphael Bryson, Daniel Joram, Sameer Abeid na Majaliwa Mbanga.
Akizungumza mara baada ya kumalizana na Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja, Ngassa ambaye alipewa jezi namba 10 iliyokuwa inavaliwa na Mahundi, alisema kuwa amekwenda Mbeya  City kwa lengo moja la kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri kwenye mechi za mzunguko wa pili wa ligi.

"Najua kuna maneno na minong'ono mingi kuhusu uwezo wangu, muda si mrefu yataisha kwa sababu najua nini nafanya, soka ndiyo maisha yangu, naomba watu wote walio nyuma ya timu hii waniunge mkono nina uhakika tutakuwa na majibu mazuri mwisho wa msimu," alisema Ngassa.

No comments:

Post a Comment