Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 24, 2016

CHEKA AGOMA KUPANDA ULINGONI KUPIGANA NA DULLA MBABE KESHO HADI APEWE PESA YAKE


Habarini za jioni mashabiki wangu poleni sanaa na majukumu Nipo Dar es Salaam Napenda kuwajurisha kesho SITAPANDA ULINGONI ifahamike hivyo na maamuzi haya nimeamua kwa kushirikiana na management yangu baada ya promota kutoonyesha ushirikiano.Ngumi ndio kazi yangu napigana ili nipate pesa sasa mtu anaandaa pambano halafu pesa ya kumlipa bondia ili apande ulingoni haijamaliziwa kwangu mpaka sasa na leo siku ya kupima uzito ndio ilitakiwa nimaliziwe malipo yang lakini hakuna kilichofanyika utaratibu wangu wa kazi huwa sipandi ulingoni bila kulipwa pesa yangu na huwa siupi nafasi ubabaishaji ktk kazi yangu.Kwa hiyo mashabiki wangu kama mtapenda mnaweza kujitokeza PTA kuwaona mabondia wengine watakaopanda ulingoni.Nawaombeni radhi mashabiki wangu nipo tayari kupigana kwa siku nyingine yoyote atakapo malizia malipo yangu.Nawatakieni sikukuu njemaa ya xmass na mwaka mpyaaa.Ahsanteni sanaa
Huu ni waraka wa Cheka alioandika kwenye ukurasa wake wa facebook.