Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 4, 2016

SIMBA NA YANGA KIBARUANI KESHO

 Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), mzunguko wa 15 unaomaliza duru la kwanza kwa msimu huu, inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu 12 kuchuana kwenye viwanja sita.

Kwa keshotwa Jumapili, African Lyon inatarajiwa kucheza na Simba kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika mchezo Na. 144 wakati Mbao itakuwa mwenyeji wa Azam FC Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika mchezo Na. 116.

Kwa upande wake, Ndanda siku ya Jumapili itakuwa mwenyeji wa Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kwenye mchezo Na 117 wakati Tanzania Prisons inatarajiwa kuialika Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika mchezo Na. 118.

Kagera Sugar kwa upande wake siku hiyo ya Jumapili itacheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, mjini Kagera katika mchezo ulipewa Na. 119 ilihali JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani kwenye mchezo Na. 120.

Ligi hiyo itaendelea Jumatatu kwa michezo miwili ambako Mtibwa Sugar itaialika Mbeya City kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Morogoro katika mchezo Na. 113 wakati Mwadui itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Mwadui huko Shinyanga katika mchezo ulipewa Na. 115.



No comments:

Post a Comment