Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 4, 2016

TEGETE AFUNGUA KITABU CHA MABAO MWADUI
MSHAMBULIAJI Jerson Tegete jana alifunga mabao mawili lakini yalishindwa kuinusuru timu yake ya Mwadui kupokea kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa kwenye  Uwanja wa Mwadui Complex.

Tegete aliyetokea benchi alifunga mabao hayo dakika ya 63 kwa mpira wa adhabu karibu kabisa na lango la Mtibwa huku lile la pili akitupia dakika ya 93 baada ya kumzidi ujanja golikipa Saidi Mohamed 'Nduda'.

Haruna Chanongo ndiye aliyefungua karamu hiyo ya mabao kwa upande wa Mtibwa katika dakika ya sita kabla ya Kelvin Friday na Rashidi Mandawa kuwamaliza 'Wachimbaji' hao wa madini ya Almasi.

Mwamuzi Jonesia Rukyaa alimtoa kwa kadi nyekundu Mandawa baada ya kupoteza muda makusudi dakika ya 74 na kuwafanya Wakata miwa hao wamalize pungufu katika robo ya mwisho ya mchezo huo.

Mchezo mwingine uliopigwa jana  Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbao FC na kufikisha alama 21 na kupaa hadi nafasi ya nne.