Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, November 16, 2016

AZAM YASAJILI WASHAMBULIAJI WAWILI TOKA GHANA


Na Rahel Pallangyo
WASHAMBULIAJI wawili raia wa Ghana, Yahaya Mohammed na Samuel Afful wamesajiliwa na klabu ya Azam FC, kwa ajili ya kuichezea timu hiyo mzunguko wa pili.
Yahaya Mohammed ambaye alikuwa anachezea timu ya Aduana Stars ameingia mkataba wa miaka miwili  na Samuel Afful ambaye alikuwa anachezea Sekondi Hassacan, amesaini mkataba wa miaka mitatu.
Mohammed ambaye anaongoza kwa upachikaji wa mabao kwenye ligi ya kwao, mpaka sasa ana mabao 15 amesema amefurahi kusajiliwa Azam FC, na kudai amekuja Azam kwa sababu ndio klabu ilionesha nia ya kumwihitaji.
“Nimekuja Azam FC kwa sababu walionesha nia ya kunihitaji na leo nimekuja kusaini mkataba nao, naamini popote ukicheza kwa bidii unaweza kuonekana na kwenda mbele zaidi”, alisema Mohammed.
Mohammed na Samuel wote wamecheza timu za taifa za Ghana kwa nyakati tofauti kuanzia zile za U-20, U-23 na timu kubwa (senior team)
Naye kocha wa Azam FC, Zeben Hernandez amesema amefurahi kupata saini za wachezaji hao kwani itasaidia kuziba pengo la wachezaji waliomaliza mikataba yao.
“Naamini mzunguko wa pili tutaanza tukiwa na uhakika wa kufanya vizuri baada ya kuwapata wachezaji hawa”, alisema Hernandez a,baye ameondoka jana usiku kwenda kwao kwa ajili ya mapumziko mafupi.