SHIRIKISHO la soka nchini Tanzania (TFF) limesema mchakato
wa ubunifu wa jezi za timu Taifa umeachwa kwa wabunifu wa mavazi pamoja na
wadau wengine.
Akizungumza
na gazeti hili Ofisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema mpango
wa ubunifu wa jezi mpya za timu za Taifa, umeibuliwa tena kutokana na mikakati
iliyowekwa na uongozi uliopo madarakani.
"Kila inapopita miaka miwili tuhakikisha kila ni
lazima timu za Taifa ziwe katika mtazamo tofauti kimavazi", alisema Lucas.
Lucas amesema
suala hilo wamemaua kulifanya kuwa wazi kwa kila mdau kushiriki kikamilifu ili
kupata muundo na muonekano mzuri wa jezi ambazo zitaanza kutumika mwaka ujao.
Muundo wa ubunifu wa jezi zinazotumika kwa sasa na timu za
Taifa ulibadilishwa na uongozi wa Rais Jamal Malinzi jambo ambalo lilizua malalamiko
kwa wadau, wakisema rangi zake hazina mvuto na hazileti utaifa.
Timu za Taifa zinatumia jezi za rangi nyeupe juu na chini
zikiwa na kola ya kijani ugenini na nyumbani zinavaa jezi za rangi ya bluu juu
na chini shingoni zikiwa na kola ya kijani.
No comments:
Post a Comment