Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, October 14, 2016

NGOME BINGWA WA MIELEKA YA KUMUENZI NYERERETIMU ya Mieleka ya Ngome, imetwaa kombe la mashindano ya mieleka ya kumuenzi baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere yaliyokuwa yanafanyika kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa.
Ngome imeibuka bingwa baada ya kupata medali za dhahabu tatu, fedha mbili na shaba tatu ikifuatiwa na JKT ambayo ilipata medali za dhahabu mbili, fedha tatu na shaba nne.
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na magereza ambao walitawala kwenye uzito wa juu ikiwa na medali za dhahabu mbili, fedha mbili na shaba moja.
Mashindano hayo ambayo yalishirikisha timu tano, yalishuhudia timu za WWC na Tanga Stars zikiondoka bila medali.
Akizungumza baada ya kukabidhi kombe kwa washindi, Mwenyekiti wa Chama cha Mieleka (AWATA) Andrew Kapelela alisema wameandaa mashindano hhayo ili kumuenzi baba wa Taifa, Julius Nyerere kwa vile alikuwa anapenda michezo.
"Sisi AWATA tumemuenzi baba wa Taifa kwa kucheza mchezo wetu na naamini kila chama na taasisi watamuenzi kwa kufanya kile kilichopo kwenye chama chao", alisema Kapelela.
Mashindano ya mieleka yalianza Octoba 10 na kuhitimishwa Octoba 13 na hufanyika kila mwaka kumuenzi baba wa Taifa, Julius Nyerere.