Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, October 15, 2016

LIVERPOOL NA MANCHESTER UNITED NANI KUCHEKA KESHO?KESHO patachimbika Anfield, ambapo watani wa jadi wa kihistoria nchini England, Liverpool na Manchester United watakabiliana kwenye mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL).
Ni wakali wawili – Jurgen Klopp na Jose Mourinho wanaokutana, huku Klopp wa Liverpool akiwa na nafuu zaidi kwa jinsi mwelekeo wa ligi unavyoendelea.
Wakati Liverpool hadi Jumamosi asubuhi walikuwa wamekaa katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 16, Man U walikuwa katika nafasi ya sita wakiwa na pointi 13 na wachezaji wa Man U wamekuwa wakilaumiwa kwa kucheza chini ya kiwango, huku kukiwa na tetesi za kutaka kuuzwa kwa nahodha wao, Wayne Rooney.
Mechi hii ya mahasimu ambayo huku Uingereza  hujulikana kama ‘derby’ na mahsusi kwa hii ni ‘North-West Derby’ kwa maana ya kwamba ni mechi ya watani wa jadi walio kwenye ukanda wa Kaskazini Magharibi ya England.
Hawa wawili katika historia ya England ndio watani wa jadi kama ilivyo Tanzania kwa Yanga na Simba. 
Hii ni mechi kubwa zaidi ya kihasimu kuliko hata kwa dhidi ya Everton ambao wapo jirani zaidi na Liverpool au hata baina ya Manchester United na Manchester City walio kwenye mji mmoja.
Uhasama huu umechangiwa, pamoja na mambo mengine, miji mikubwa wanakotoka timu hizi, kwani ndiyo majiji makubwa ya hapa England – Liverpool na Manchester yakitanguliwa na London. 
Kadhalika historia ya uchumi wao na mchuano wa kiviwanda unachangia kwa kiasi kikubwa kuupa utamu utani wao huu.
Hizi ni timu kubwa kwa hakika, zikiwa zimepata heshima ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kupata ubingwa nyumbani na Ulaya na kuwa na washabiki wengi hata ng’ambo,
Ukiwachanganya kwa pamoja wamepata kutwaa makombe 38 ya ligi hapa nyumbani, manane ya Ulaya, matatu ya Uefa, moja la Kombe la Dunia la Klabu, moja la Intercontinental Cup na 36 ya FA kwa Ngao ya Jamii.

Timu hizi kijiografia zipo umbali wa maili 35 na tangu wakati ule wa mapinduzi ya viwanda pamekuwapo msuguano na utani baina yao kuhusiana na masuala ua uchumi na viwanda, kila mji ukijidai kwamba upo juu ya mwingine.
Katika karne ya 18 Manchester ilikuwa juu zaidi na kuonekana kama ndiyo kioo cha ukanda wa Kaskazini lakini Liverpool hawakuwa wakipenda hilo.
Kwa upande mwingine ni kwanba Liverpool ilikua moja ya miji mikubwa ya bandari huku kukiwa na ukuaji wa masuala ya viwanda vya nguo.
Kutokea kwa Vita ya I ya Dunia kulivuruga soka ya hapa nyumbani, ambapo mashindano yalianza tena 1919 ambapo Liverpool walikuwa juu huku United wakishuka na kuja kushushwa daraja 1923 na kuwa huko chini kwa misimu mitatu.
Wakati Man U wakipata uthabiti mwaka 1947, Liverpool walishuka daraja huku United wakiwa chini ya nahodha wa zamani wa Liverpoo, Matt Busby, na kutwaa Kombe la FA 1948.
Baadaye walikuja kutwaa makombe matatu ya Ngao ya Hisani. Ni hapo Mwenyekiti wa Liverpool, Tom Williams alimfuata Bill Shankly na kumuuliza ni utayari gani aliokuwa nao kwa ajili ya kuifundisha ‘klabu kubwa zaidi England?” yaani Liverpool, naye akamuuliza “Kwa nini? Matt Busby anaondoka?”
Kweli aliondoka na Shankly akachukua mikoba akawapandisha daraja Liverpool kuwarudisha juu walikokuwa.
Kesho wanakutana wakiwa na makocha tofauti, Liverpool wakiwa na kocha mpya kwa msimu wa pili sasa, akiwa ametoka Borussia Dortmund wakati Man United wanaye kocha mpya kwa msimu wa kwanza, akiwa alifukuzwa Chelsea kwa kufanya vibaya mno msimu uliopita.
Wote ni watambaji lakini Klopp anajulikana kwa kuwajenga vyema Liver huku Mourinho akianza vyema ligi lakini wachezaji wake bado wanamchanganya, ama hajaweza kuwapa mfumo mzuri au kuwapanga ipasavyo kwenye namba husika.