LIGI daraja
la pili inatarajiwa kuanza Octoba 29 na kushirikisha timu 24 ambazo
zimegawanywa katika makundi manne.
Akizungumza
na wandishi wa habari, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF),
Alfred Lucas, alisema raundi ya kwanza itamalizika Desemba 18 na raundi ya pili
itaanza Desemba 31 na kumalizika
Februari 5.
" Ligi
hii imepangwa kulingana na eneo au sehemu timu zinapotoka ili kupunguzia timu
gharama", alisema Lucas
Pia Lucas
alisema kundi A lina timu za Bulyankulu ya Shiyanga, Green Warriors ya Pwani ,
Mirambo ya Tabora, Mji Mkuu ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na Mashujaa ya
Kigoma
Kundi B lina
timu za AFC, JKT Oljoro, Madini FC na Pepsi zote za Arusha, African Wanderers
ya Iringa na Kitayosa FC ya Kilimanjaro
Kundi C
linaundwa na timu za Abajalo FC, cHANGANYIKE fc, Cosmopolitan FC na Villa Squad
zotw za Dar es Salaam, Bukinafaso ya Morogoro na Kariakoo ya Lindi
Kundi D lina
timu za Mawenzi FC, Mkamba Rangers na Sabasaba FC za Morogoro, Mbarali United
ya Mbeya, Namungo FC ya Lindi na The Might
Elephant ya Ruvuma.
Wakati huo
huo Lucas amewataka viongozi wa timu za daraja la kwanza kuhakikisha wanachukua
kadi za usajili za wachezaji wao kwani kuanzia mzunguko wa tano hakuna mchezaji
ambaye ataruhusiwa kucheza bila kuwa na kadi halisi ya usajili wa msimu huu.
No comments:
Post a Comment