Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 19, 2016

KICHUYA MCHEZAJI BORA SEPTEMBA




WINGA Shiza Kichuya anayechezea timu ya Simba amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu kwa mwezi Septemba msimu wa 2016/17.

Mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar ambaye amekuwa tegemeo la Wekundu hao kutokana na ubora alionao kwa sasa aliwashinda Adam Kingwande wa Stand United na Omari Mponda wa Ndanda FC.


Kichuya aliisadia timu yake kwa mwezi huo kupata pointi zote 12 katika mechi nne ilizocheza, matokeo ambayo yameifanya Simba iendelee kuongoza Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16. Pia alifunga mabao matatu katika mechi mbili kati ya nne ilizocheza timu yake.


Kwa kushinda tuzo hizo ya mwezi, Kichuya atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.

No comments:

Post a Comment