WAKATI
tiketi za elektroniki zitaanza kujaribiwa kesho, kampuni mbalimbali zimechangia
jumla ya Sh milioni 20 kwa ajili ya kudhamini mchezo wa wabunge mashabiki wa
Yanga na wale wa Simba utakaofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi.
Kampuni hizo ni Mwananchi
Communication iliyotoa Sh milioni 10, Mfuko wa Bima ya Afya, NHIF na Jubilee
Insurance, ambazo zote zimetoa Sh milioni 5 kila moja.
Akizungumza na waandishi wa
habari jana, Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Bunge, William Ngeleja ambaye
pia ni mnazi wa Simba alisema matokeo ya mchezo wa kesho ni ishara ya matokeo
ya mchezo wa Oktoba Mosi.
Kwa upande wa tiketi za
elektroniki zitaanza kutumika leo katika mechi ya wabunge mashabiki wa Simba na
Yanga kama majaribio kabla ya kuanza kutumika rasmi Oktoba Mosi katika mchezo
wa wapinzani Simba na Yanga.
Akizungumza jana, Meneja
Miradi wa Kampuni ya Selcom ambayo ndiyo iliyopewa jukumu la kusimamia mfumo
huo, Gallus Runyeta alisema kadi hizo
zitatolewa bure katika mchezo wa leo ikiwa ni
majaribio na kuangalia dosari ambazo zitajitokeza kabla ya kuanza
kuzitumia rasmi.
Akizungumzia jinsi ya
kuitumia kadi hiyo, Runyeta alisema “Utajisajili kwa kupiga *150*50# halafu ni
lazima uiwekee pesa kwa Airtel au M-Pesa.
Kiwango cha chini cha
kuongeza salio ni Sh 1,000….: “ “Unaweza ukanunua mechi moja kwa kuandika
tarehe na mchezo husika au ukachagua baadhi ya mechi au ukanunua mechi zote za
msimu za timu unayoipenda.
Aliongeza: “Mbali na kadi
hizo kuzitumia uwanjani, pia aliyenayo anaweza kuitumia kwa matumizi mengine
kama vile kuhifadhi na kutoa fedha kwa wakala, lakini pia inamwezesha mtu huyo
kulipia bidhaa na huduma mbalimbali bila kuwa na fedha mfukoni,” alisema.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan 'Zungu'
alisema
No comments:
Post a Comment