Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), imepanga mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Young
Africans dhidi ya JKT Ruvu, sasa utachezwa Oktoba 26, 2016 kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar s Salaam.
Pamoja na mchezo huo, imefanya mabadiliko katika baadhi ya ya michezo
ya Ligi Kuu ya Vodacom kama ifuatavyo ambako Mwadui na Azam sasa
utachezwa na Novemba 9, 2016 siku ambayo Prisons itaikaribisha Simba
kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Novemba 10, kutakuwa na mchezo
kati ya Young Africans dhidi ya Ruvu Shooting jijini Dar es Salaam.
Kadhalika Young African na Mtibwa sasa utachezwa Oktoba 13, 2016
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Kagera Sugar itacheza na
Azam Oktoba 28, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjimi Bukoba huku Young
Africans dhidi ya Mbao utapigwa Oktoba 30, 2016 jijini Dar es Salaam
wakati Toto Africans na Mtibwa Sugar watakutana Oktoba 30, 2016 kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Mtibwa Sugar na Mbeya City itachezwa Novemba 7, 2016 kwenye Uwanja wa
Manungu huko Mvomero, mkoani Morogoro wakati Mwadui na Majimaji
itachezwa tarehe hiyohiyo huko Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kambarage
wakati Oktoba 7 kutakuwa na mchezo kati ya Mbeya City na Stand United
kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
No comments:
Post a Comment