Mwanariadha
kutokea nchini Jamaica, Usain Bolt, amedhihirisha kwamba yeye ni mwamba
wa mbio za Mita fupi mara baada ya kushinda Mita 200 katika michuano ya
Olimpic inayofanyika huko Rio nchini Brazil na kujinyakulia medali ya
Dhahabu ikiwa ni mara ya pili baada ya kunyakua ya michuano yam bio za
Mita 100.
Bolt
aliweza kushinda mbio hizo kwa urahisi kwa kutumika Sekunde 19.79 na
kwa sasa anahitaji kushinda mbio za mita 400 za kupokezana vijiti ili
kukamilisha medali ya tatu ya dhahabu kama alivyofanya katika michuano
iliyopita.
Mapema wiki hii alidhihirisha kuwa ni mwamba wa mbio fupi pale aliposhinda mbio za mita 100 na kunyakuwa medali ya dhahabu.
Kwa upande wa Marekani imeweza kujinyakulia medali nyingine nne za Dhahabu ikiwemo ya mwanariadha wake Ashton Eaton.
Huku
mkimbiaji kutokea nchini Kenya aliyekuwa ametangaza kustaafu, Ezekiel
Kemboi, ameeleza kwamba ameahirisha kustaafu mara baada ya
kunyang`anyway medali aliyokuwa ameshinda katika mbio za kuruka viunzi
na maji.
Medali
hiyo iliyochukuliwa na Mfaransa mara baada ya kukata Rufaa kwenye Mita
3000 imemfanya Kemboi kusema kuwa watakutana tena London 2017 kwenye
michezo ya Olimpiki ili kuweza kudhihirisha kwamba alikuwa akistahili
medali hiyo.
No comments:
Post a Comment