Katika
kuhakikisha wanaboresha mashindano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya
(UEFA Champions League), Chama cha Soka Ulaya (UEFA) limepanga kufanya
maboresho ya idadi ya timu ambazo zitakuwa zinafuzu ili kuhakikisha
zinapita timu bora.
Mabadiliko
hayo ni kuchukua moja kwa moja timu nne kutoka katika ligi nne bora
barani humo kuingia katika hatua ya makundi tofauti na sasa ambapo
mataifa yote timu inayoshika nafasi ya nne katika ligi yao inacheza
kwanza michezo ya awali ili kupata nafasi ya kutinga hatua ya makundi.
Mpango
huo umekuja baada ya Kamati ya Mashindano ya UEFA kukutana kujadili ni
jinsi gani watazifanya ligi kubwa Ulaya zinasalia kuwa ligi bora na timu
zao zipate nafasi kubwa ya kushiriki ligi ya mabingwa tofauti na vilabu
ligi zingine.
Mabadiliko hayo yatazihusisha timu zinazotoka ligi nne bora Ulaya ambazo ni Uingereza, Ujerumani, Hispania na Italia.
No comments:
Post a Comment