SIMBA
imeanza kwa kishindo Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa
mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara katika mchezo uliofanyika kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao yote
ya Simba yamewekwa kimiani na wachezaji wake waliosajiliwa katika dirisha la
usajili lililomalizika hivi karibuni.
Ushindi huo
umeifanya Simba kuondoka na pointi tatu muhimu na kupeleka raha kwa mashabiki
wa timu hiyo, ambao kwa miaka kadhaa walikosa raha kwa timu yao kufanya vibaya.
Mshambuliaji
mpya wa Simba, Laudit Mavugo alifunga katika dakika ya 19 baada ya kuunganisha
mpira wa adhabu uliopigwa na Mohamed Hussein `Tshabalala’.
Hatahivyo,
Omary Mponda wa Ndanda aliisawazishia timu yake kwa bao la dakika ya 36 kwa
kichwa akiunganisha wavuni mpira wa adhabu uliopigwa na Kiggy Makassy.
Simba
walizidi kukaribia ushindi baada ya kupata bao la pili lililofungwa na mchezaji
wake wa Ivory Coast, Frederic Blagnon aliyeingia akitokea benchi kuchukua
nafasi ya Mohamed Ibrahim.
Wekundu hao
wa Msimbazi walijihakikishia ushindi baada ya kufunga bao la tatu kupitia kwa
Shiza Kichuya katika dakika ya 74 baada ya kuunganisha mpira wa kona uliokolewa
na kurudi uwanjani na kumkuta mfungaji aliyechia kiki kali.
Kikosi Simba:
Vicent
Angban, Malika Ndeule, Mohamed Hussein, Method Mwanjale/Mwinyi Kazimoto, Juuko
Murshid, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim/
Frederic Blagnon, Laudit Mavugo, Ibrahim Ajib na
Jamal Mnyate.
Katika mchezo mwingine; Ruvu Shooting iliifunga Mtibwa Sugar
bao 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Manungu Turiani.
Nayo Stand
United ilitoka suluhu na Mbao FC katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Tanzania
Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Prisons
imeondoka na pointi zote tatu baada ya kuidungua Majimaji ya Songea katika
mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment