Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 20, 2016

GUARDIOLA AMKACHA JOE HART


WEB ILIYOSHE
MENEJA wa Manchester City Pep Guardiola amesema kipa wao Joe Hart anaweza kuondoka akitaka.
Tangu atue Guardiola hapo City, Hart amepigwa Benchi na namba yake kuchukuliwa na Kipa kutoka Argentina Willy Caballero ambae amedaka Mechi zote 2 za Masimu mpya.

Caballero alicheza wakati City inaifunga Sunderland kwenye Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England, EPL, Wikiendi iliyokwisha na pia kudaka Alhamisi Usiku wakati City inaitandika Steau Bucharest 5-0 huko Romania kwenye Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONS LIGI.

Inasemekana Hart, mwenye Miaka 29 na Kipa Namba Wani wa England, anatafakari kuondoka City acheze kwa mkopo kwingine na Guardiola amesema: “Sitaki Wachezaji wabaki kama hawataki. Wakitaki kubaki wabaki na kupigania namba.”
Hivi sasa kuna minong’ono City ipo mbioni kumnasa Kipa na Makipa wa Barcelona Claudio Bravo na Marc-Andre ter Stegen wanatajwa.