Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, July 25, 2016

ARSENAL KUNUNUA WACHEZAJI 2 KWA MPIGO NA MOYES ALILIA MCHEZAJI WA MAN UNITED

Arsenal wanatafakari kumwaga Dau la Jumla ya Pauni Milioni 75 kumnunua Winga wa Leicester City Riyad Mahrez, mwenye Miaka 25, na Straika wa Lyon Alexandre Lacazette ambae pia ana Miaka 25.
Nao Swansea City wapo njiani kumsaini tena Straika wao wa zamani Wilfried Bony, mwenye Miaka 27, ambae sasa yupo Man City.
Nae Straika wa Everton, Romelo Lukaku, mwenye Miaka 23, anawania kurejea tena Chelsea.

Winga wa Marseille Georges-Kevin N'Koudou, 21, anakaribia kukamilisha Uhamisho kwenda Tottenham na yeye anamfuatia Straika wa Netherlands Vincent Janssen, 22, ambae tayari yupo White Hart Lane.

Meneja pya wa Sunderland manager David Moyes anataka kumsaini Straika Will Keane, 23, kutoka Manchester United kwa Dau la Pauni Milioni 6.5.

Wakati huo huo, Wapinzani Manchester United na Manchester City wametumbukia kwenye mvutano wa kumuwania Straika Chipukizi wa Brazil Gabriel Jesus, 19.
Habari nyingine zimeripoti kuwa Kiungo wa Man United Bastian Schweinsteiger, 31, anaweza kuwa mmoja wa Wachezaji wa Klabu hiyo ambao watauzwa na wengine wakitajwa kuwa ni Juan Mata, 28, na Memphis Depay, 22.