Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 30, 2016

SIR ALEX AMSIFU WENGER KWA MSIMAMO ENGLAND

MENEJA wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson amemsifu mpinzani wake wa zamani Arsene Wenger kwa kuwa na msimamo thabiti licha ya kushinikizwa na presha kubwa kutoka kwa Mashabiki wa Arsenal na Wanahabari wa England.
Ferguson ameisifia himaya ya Wenger huko Arsenal na kutobadilika kwake licha ya kusakamwa na wapondaji.
Msimu huu, Wenger alikuwa na presha kubwa ya kupondwa sana baada ya Arsenal kuanza vyema Ligi Kuu England na mwishowe kutoweka kwenye mbio za Ubingwa ambapo hatimae Leicester City waliutwaa.
Wadau wengi wamekuwa wakidai Wenger anaifanya Arsenal idorore kwa kushindwa kununua Mastaa waliojengeka wa Bei mbaya na badala yake huchukua Vijana wa bei chee tu.
Lakini Ferguson amedai Wenger anastahili pongezi kwa kushikilia falsafa yake.

Akiandika kwenye Makala maalum ya UEFA CHAMPIONS LIGI, Ferguson alisema; "Amekuwa hodari. Sasa anapondwa lakini nahusudu msimamo wake wa kutoyumba licha ya kupondwa. Amebaki na kile anachoamini. Watu wanaofanya hivyo ni Makocha waelewa!"
Aliongeza: "Wenger hajabadili uchezaji wa Timu. Alipofika alirithiki Wachezaji kama Steve Bould, Martin Keown na Tony Adams lakini Timu yake ilibadilika walipoingia kina Thiery Henry, Robert Pires, Emmanuel Petit na Sylvain Wiltord. Utamaduni wa Timu ulibadilika."
"Ikawa Timu kali na uzoefu aliopata na Timu hiyo umemfanya asibadilike kuhusu aina ya Mchezaji anaemtaka na uchezaji anaotaka. Siku zote ni Mipira ya kupasua Difensi huku Wachezaji wakichomoka kwenye nafasi safi, pasi nzuri kwenye engo kwa Mastraika!