Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 30, 2016

MABINGWA MADRID WATUA NYUMBANI MADRID NA KUPATA MAPOKEZI MAKUBWA

Mabingwa wa Uefa Champions League kwa mara ya 11, Real Madrid wamerejea kwao Hispania na kupokelewa kwa shangwe ile kinoma. Madrid wamerejea katika jiji la Madrid saa chache baada ya kubeba ubingwa huo kwa mikwaju 5-3 ya penalti dhidi ya wapinzani wao wakubwa Atletico Madrid. Mechi ya fainali ilichezwa katika jiji la Milan, kwenye Uwanja maarufu wa San Siro na mechi hiyo kutazamwa na zaidi ya watu milioni 200 duniani kote. 
Leo hii Asubuhi walitua kwao Jijini Madrid na kulitembeza Kombe Mitaani.
Maelfu ya Mashabiki wao walijimwaga Barabarani kushuhudia Mabingwa wao wakipita kwenye Basi la wazi na Taji lao.
Hii ni mara ya pili katika Miaka Mitatu kwa Real kuibwaga Atletico na kutwaa Kombe la UEFA CHAMPIONS LIGI.