SHIRIKISHO la Soka Afrika limetaja mfumo mpya wa
mashindano yake kuanzia mwakani, na sasa limerudisha mtindo wa mechi za mtoano
kuanzia hatua ya robo fainali.
Kamati ya Mashindano ya CAF ilikubaliana juu ya mfumo mpya wa Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.
Mabadiliko katika mashindano hayo mawili yalitangazwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou katika Mkutano Mkuu wa 38 wa shirikisho hilo uliofanyika mjini Mexico City, kwamba kuanzia mwakani kutakuwan na timu 16 katika hatua ya makundi.
Baada
ya raundi za awali, timu 32 zitafuzu kuwania hatua ya 16 Bora ya mashindano
yote.
Watakaofuzu hatua ya 16 Bora kwa Ligi ya Mabingwa
wataingizwa moja kwa moja katika makundi manne. baada ya mechi za makundi za
nyumbani ugenini, washindi wawili wa juu wa kila kundi wataingia Robo Fainali
ambayo itaanza kuchezwa kwa mtoano pia hadi fainali.
Klabu
zitakazoongoza makundi zitaanzia ugenini katika Robo Fainali na kumalizia
nyumbani.
Katika Kombe la Shirikisho, timu 16 zitakazofuzu hatua ya makundi zitakuwa ni pamoja na zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa na baada ya hapo, mambo yatakwenda kama yalivyopangwa kwenye Ligi ya Mabingwa.
Katika Kombe la Shirikisho, timu 16 zitakazofuzu hatua ya makundi zitakuwa ni pamoja na zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa na baada ya hapo, mambo yatakwenda kama yalivyopangwa kwenye Ligi ya Mabingwa.
CAF
sasa ina tarehe 20 za kalenda ya mashindano hayo ambayo yataanza Marchi hadi
Novemba kwa Ligi ya Mabingwa na hadi Desemba.
No comments:
Post a Comment