Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, May 12, 2016

CAF KUONGEZA IDADI YA TIMU KWENYE MASHINDANO YAKE

Shirikisho la vyama vya soka Afrika CAF limepanga kuipanua michuano yake ya ngazi za Klabu, ile ya Klabu bingwa na ile ya Shirikisho katika hatua ya makundi kutoka timu nane za sasa mpaka kumi na sita ifikapo mwaka 2017. Hayo yamesemwa jana Jumatano huko Mexico na Rais wa shirikisho hilo Issa Hayatou wakati akiongea na wakuu wa soka toka Afrika wanaohudhuria mkutano wa FIFA unaoendelea nchini humo. Hayatou amesema muundo huo mpya utashirikisha makundi manne madogo madogo ya timu nne nne badala ya muundo wa sasa ambao umekuwa ukishirikisha makundi mawili ya timu nne nne ambapo washindi wa kwanza na wa pili wa kila kundi hufuzu hatua ya nusu finali. Wakati huohuo Hayatou amesema kuwa muundo huo mpya utaenda sambamba na uboreshwaji wa zawadi za fedha kwa washindi wa michuano hiyo hii ni baada ya CAF kuingia mkabata mpya wa miaka 12 wa matangazo na masoko [Media and Marketing] wenye thamani ya zaidi ya dola Bilioni moja. Kwa sasa mshindi wa Ligi ya mabingwa hupata kitita cha dola milioni $1.5 na bingwa wa Shirikisho hupata dola $660,000.


No comments:

Post a Comment