Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, May 13, 2016

AZAM FC YALETA MAKOCHA WAPYA LEO



Kocha Mkuu mpya wa Azam FC, Zeben Hernandez (kushoto) na msaidizi wake Jonas Garcia (kulia) raia wa Hispania wakiwa na Mtendaji  Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba aliyekuja kuwapokea baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) jana. Hernandez amekuja kuchukua nafasi ya Stewart Hall. (Picha na Rahel Pallangyo)





KOCHA Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez amesema amefurahi kuja Tanzania kwani anaamini kuna vipaji kama Farid Mussa anayecheza soka Hispania.
Zeben Hernandez ambaye atakuwa kocha Mkuu endapo watakubalia na uongozi wa Azam FC, atakuwa akisaidiwa na Jonas Garcia walipokelewa leo na Saad Kawemba Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA)
Makocha hao ambao  raia wa Hispania wametoka klabu ya Deportivo Tenerife ya nchini humo.
Akizungumza na gazeti hili wakala wa makocha hao Rayco Garcia alisema kuwa makocha hao wamevutiwa kuja Tanzania baada ya kuona kiwango cha mshambuliaji Farid Musa ambaye amesajiliwa na klabu hiyo ya daraja la kwanza akitokea Azam FC.
“Makocha hawa wamekuja Tanzania baada ya kuridhishwa na kiwango cha mchezaji Farid na wanaamini kuna vipaji vingi,” alisema Rayco
Makocha hao watasafiri kwenda Tanga leo kuiona Azam FC, ikicheza na African Sports katika mchezo wa Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Tayari kocha Muingereza, Stewart John Hall amekwishaaga kwamba ataondoka mwishoni mwa msimu, ambao unakamilika Juni.









No comments:

Post a Comment