Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 18, 2016

YANGA NA APR ZATAMBIANA

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm (kulia) akizungumza na wandishi wa habari kuhusu mchezo wa klabu bingwa dhidi ya APR utakaochezwa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kushoto ni Kocha Mkuu wa APR, Nizar Kanfir. (Picha na Rahel Pallangyo)


MAKOCHA wa Yanga na APR wametamba kila mmoja timu yake kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa marudiano raundi ya kwanza wa klabu bingwa Afrika, utakaochezwa  kesho Uwanja wa Taifa
Akizungumza kwa kujiamini kocha wa APR,  Nizar Kanfir, alisema mchezo wa kwanza walifungwa mabao 2-1 na sasa ni zamu yao kurudisha kipigo hicho kutokana na maandalizi waliyoyafanya.
“Yanga ni timu nzuri walitufunga kwetu kwenye dakika 90 za kwanza sasa ni zamu yao nao kufungwa kwani tunahitaji kusonga mbele na siyo kukamilisha ratiba,” Kanfir.
Naye Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema katika mchezo huo watashambulia kusaka mabao zaidi na kukosekana kwa Juma Abdul siyo tatizo kwao.
“Wachezaji wana ari hivyo naamini tutashinda mchezo dhidi ya APR hivyo tunawaomba mashabiki waje kwa wingi kuishangilia timu yao,” alisema Pluijm
Juma Abdul ambaye ndiye aliyefunga bao la kwanza katika mchezo wa awali uliochezwa Kigali, Rwanda atakosa mchezo wa marudiano kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano.
Wakati huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri klabu wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, timu za Azam FC, JKU na Yanga katika michezo yao watakayocheza wikiendi hii.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Afisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto, alisema TFF imezitaka timu zote kuhakikisha zinafanya vizuri katika michezo yao ili ziweze kusonga mbele katika hatua inayofuata, na kuwapa furaha washabiki wa mpira wa miguu pamoja na watanzania wote.
Yanga watakua wenyeji wa APR ya Rwanda katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa (CAF CL) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam, mchezo utakaochezeshwa na mwamuzi Bernard Camille, akisaidiwa na Eldrick Adelai, Gerard Pool na Allister Bara kutoka nchini Shelisheli.
Kesho Azam FC watacheza na Bidvest FC kutoka nchini Afrika Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (CAF CC) kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, mwamuzi wa mchezo huo ni Gait Oting akisaidiwa na Abdallah Gassim, Casim Dehiya, mwamuzi wa akiba Ariel James wote kutoka Sudan Kusini