Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, March 19, 2016

YAMGA YAFUZU RAUNDI YA PILI LICGHA YA KUTOKA SARE NA APR







YANGA imefuzu raundi ya pili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayoshirikisha timu 16 bora kwa kuitoa APR ya Rwanda jumla ya mabao 3-2.
Hatua hiyo inatokana na sare ya bao 1-1 katika mchezo wa leo baina ya timu hizo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliofanyika wiki iliyopita Uwanja wa Amahoro, Kigali, Yanga ilishinda mabao 2-1, hivyo jana ilikuwa ikihitaji sare ama isifungwe zaidi ya bao 1-0 ili ifuzu.
Kutokana na matokeo hayo, Yanga sasa itamenyana na mshindi wa mchezo kati ya Al Ahly ya Misri na Recreativo de Libolo ya Angola uliotarajiwa kufanyika jana Cairo, Misri.
Mchezo wa kwanza uliofanyika Luanda, Angola timu hizo hazikufungana, hivyo timu itakayopenya itacheza hatua ya 16 Bora kwa kupambana na Yanga.
Tofauti na wengi walivyodhania kwamba APR ingekuwa timu nyepesi, jana iliwaduwaza mashabiki baada ya kupata bao la mapema dakika ya tatu likifungwa na Fiston Nkinzingabo akiunganisha krosi ya Jean Iranzi.
Bao hilo lilionekana kuwachanganya Yanga na kufanya mashambulizi ya nguvu, lakini umaliziaji haukuwa mzuri.
Yanga ilisawazisha bao dakika ya 27 mfungaji akiwa Donald Ngoma baada ya kuwalamba chenga mabeki wa APR na kufumua shuti lililotinga wavuni.
Washambuliaji wa Yanga na APR walipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini umaliziaji haukuwa mzuri kwa kushindwa kulenga lango.
Yanga; Ally Mustafa Barthez, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Pato Ngonyani, Deus Kaseke/Geoffrey Mwashiuya, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Haruna Niyonzima/Simon Msuva. 

APR: Jean Claude Ndoli, Rusheshangonga Michael, Rutanga Eric, Rwatubyaye Abdul, Emery Bayisenge, Yannick Mukunzi, Fiston Nkinzingabo/Djihad Bizimana, Benedata Janvier/Bertrand Iradukunda, Issa Bigirimana, Iranzi Jean Claude na Patrick Sibomana.
Wakati huohuo, wawakilishi wengine wa Tanzania katika michezo ya kimataifa timu ya Azam FC, leo wanashuka Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam wakicheza dhidi ya Bidvest FC kutoka nchini Afrika Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (CAF CC) .
Waamuzi wa mchezo huo ni Gait Oting akisaidiwa na Abdallah Gassim, Casim Dehiya, mwamuzi wa akiba Ariel James wote kutoka Sudan Kusini, ambapo mchezo wa kwanza uliofanyika Afrika Kusini, Azam ilishinda mabao 3-0. Kwa mazingira hayo Azam leo itahitaji sare ya aina yoyote au isifungwe zaidi ya mabao 2-0.

No comments:

Post a Comment