Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 4, 2016

SIMBA KUIVAA COASTAL UNION WAKATI YANGA WAKIJIULIZA KWA NDANDA FC KOMBE LA FA


RATIBA ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho  inatarajiwa kuchezwa wikiendi ya mwisho wa mwezi Machi, ambapo Yanga itacheza na Ndanda na Simba itaivaa Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Baraka Kizuguto alisema timu nane zitachuana kusaka nafasi ya kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
“Timu nane zilizofuzu kwenye robo fainali zitacheza mwisho wa mwezi Machi, kusaka tiketi ya nusu fainali,” alisema Kizuguto
Machi 26, wachimba dhahabu, Geita Gold FC, watakuwa wenyeji wa wachimba Almasi, timu ya Mwadui FC katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Machi 31, Yanga watawakaribisha Ndanda FC katika Uwanja wa Taifa, Dar es salaam na Azam FC watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Simba na Coastal Union watacheza robo fainali ya mwisho Aprili 6, katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Baada ya michezo ya robo fainali kumalizika, Aprili 7 itachezeshwa droo ya hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, mojamoja katika Luninga (live).
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho msimu huu, ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) 2017.