
Conte, mwenye Miaka 46, ni Meneja wa Timu ya Taifa ya Italy na Mkataba wake unamalizika mara baada ya kwisha kwa EURO 2016 mapema Mwezi Julai.

Kwa mujibu wa Jarida la Italy, Corriere dello Sport, Abramovich amewahakikishia Wachezaji wa Chelsea kuwa Conte ndie Meneja mpya wakati alipokutana na Kikosi chote kwenye Kituo cha Mazoezi cha Timu hiyo huko Cobham Mjini London.
Hivi sasa Chelsea wana Meneja wa muda Guus Hiddink ambae Mkataba wake unamalizika mwishoni mwa Msimu baada ya kuteuliwa kuchukua nafasi ya Jose Mourinho alieondolewa Mwezi Desemba.
Tangu wakati huo, Hiddink ameisimamisha wima Chelsea na kupanda kwenye Ligi Kuu England hadi Nafasi ya 10 toka Nafasi za mkiani Mwezi Desemba ikiwa sasa Pointi 8 tu nyuma ya Timu ya 4 kwenye Ligi.
No comments:
Post a Comment