Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 4, 2016

MARCUS RASHFORD APATA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI WA MAN UNITED

CHIPUKIZI Marcus Rashford ameshinda Tuzo ya Manchester United ya Mchezaji Bora kwa Mwezi Februari baada ya kufunga Mabao muhimu katika Mechi dhidi ya FC Midtjylland na Arsenal zikiwa ni Mechi zake za kwanza kabisa kuchezea Kikosi cha Kwanza.
Rashford, mwenye Miaka 18 na ambae amekulia Kisoka kutoka Chuo cha Man United, alizoa Kura Asilimia 56 zilizopigwa na Mashabiki kumteua Mshindi kwenye Tovuti ya Man United na Akaunti ya Klabu hiyo ya Twitter huku akiwabwaga Memphis Depay, aliepata Asilimia 31, na Jesse Lingard, Asilimia 13.
Licha ya kucheza Mechi 2 tu kati ya 7 Man United walizocheza Mwezi Februari, mchango wake mkubwa katika Mechi hizo mbili ambazo Man United walitakiwa kushinda za UEFA EUROPA LIGI na Ligi Kuu England ulikuwa mkubwa mno kwa Magoli yake Manne na kutengeneza Bao moja.
Kuibuka kwa Kinda huyo kumeleta afueni na faraja kubwa kwenye Kikosi cha Man United chini ya Meneja Louis van Gaal na Msaidizi wake Ryan Giggs kitu ambacho pia kimesifiwa na Wachezaji wakubwa wa Timu hiyo.
Michael Carrick, ambae ni Makamu Nahodha, alieleza: “Ni Kijana adhimu na mpole. Ujio wake umeleta mabadiliko mapya!”
Nae Morgan Schneiderlin amemsifia Rashford na kusema ingawa hajafanya nao mazoezi mara nyingi lakini alipojumuika nao moja kwa moja alionyesha ana kipaji kikubwa.
Kuibuka kwa Rashford na kuingizwa kwenye Timu kulikuja Dakika za mwisho baada ya Mastaa Wayne Rooney, Anthony Martial na Kijana mwingine Will Keane wote kuumia.