Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 23, 2016

TUHUMA ZA UPANGAJI WA MATOKEO DARAJA LA KWANZA KUANZA KUSIKILIZWA MACHI 20


KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) itakutana Machi 20 kusikiliza sakata la upangaji wa matokeo unaozihusisha timu nne za daraja la kwanza.
Akizungumza na wandishi wa habari, Rais wa Shirikisho la soka Tanzania, Jamal Malinzi, alisema kuwa TFF imegeuka kuwa mlalamikaji kwenye sakata hilo linalozihusisha mchezo kati ya timu za JKT Kanembwa dhidi ya  Geita Gold SC, na Polisi Tabora na JKT Oljoro.
"Ndugu zangu swala la upangaji matokeo linahitaji ushahidi hivyo sisi TFF kama walalamikaji tumelipeleka kwenye kamati ya nidhamu na tumewataarifu wahusika kwa maana ya pande zote ikiwemo waamuzi," alisema Malinzi
Awali Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi ya Ligi maarufu kama Kamati ya Saa 72 ilikutana Februari 16, 2016 kupitia taarifa za mechi mbili za Kundi C la Ligi Daraja la Kwanza kati ya JKT Kanembwa na Geita Gold SC, na Polisi Tabora na JKT Oljoro na baada ya kupitia taarifa hizo na vielelezo vingine, Kamati  hiyo ilionyesha mashaka kutokana na kuwepo viashiria vya upangaji wa matokeo.
JKT Kanembwa ilifungwa mabao 8-0 na Geita Gold SC katika mechi iliyofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, wakati Polisi Tabora ilishinda mabao 7-0 dhidi ya JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora.

No comments:

Post a Comment