Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 10, 2016

SIMBA NA YANGA MCHELEA KOMBE LA SHIRIKISHO RAUNDI YA 16

SIMBA na Yanga zimepangwa na timu za daraja la pili na la kwanza kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho  maarufu kama Azam Sports Federation Cup.
Akizungumza na wandishi wa habari, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania Baraka Kizuguto alisema jumla ya timu 16 zinakutana katika hatua  hiyo itakayoanza kutimua vumbi Februari 26-1 Machi 2015 katika viwanja mbalimbali nchini.
“Michuano ilishirikisha timu 64 kutoka Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili, inaingia katika mzunguko wa nne huku kukiwa na timu kutoka katika ngazi zote za ligi za TFF jambo ambalo linamaanisha kuwa kuna ushindani wa kutosha,”alisema Kizuguto
Februari, 26  Ndanda FC watawakaribisha JKT Ruvu katika Uwanja wa Nang’wanda Sijaona Mtwara, huku Coastal Union wakiwa wenyeji wa wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Februari 27, Mwadui FC watawakaribisha Rhino Rangers katika Uwanja wa Mwadui Complex Shinyanga na Tanzania Prisons watacheza na mshindi kati ya Mbeya City/Wenda FC kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Februari 28, michezo mitatu itachezwa ambapo Simba watawakaribisha Singida United katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Panone FC watacheza dhidi ya Azam FC Uwanja wa Ushirika, Moshi, huku Toto African wakicheza na Geita Gold katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Raundi hiyo itamalizika Machi 1, kwa Yanga kuikaribisha JKT Mlale katika Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho mwaka huu ataiwakilisha Tanzania kwenye Mashindano ya kombe la Shirikisho Barani Africa (CAF CC) mwakani 2017.

No comments:

Post a Comment