Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 19, 2016

NAPE AMWONDOA LIHAYA BMT, ARUDISHWA WIZARANI KUPANGIWA MAJUKUMU MENGINE


Waziri Nape akiongea na wandishi wa habari leo, kulia ni Mwenyekiti wa BMT, Dioniz Malinzi na kushoto ni Katibu wa BMT, Henry Lihaya ambaye aneondolewa na Nape


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Nape Nnauye ametengua uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzani,  Henry Lihaya baada ya kushindwa kutekeleza wajibu wake. 

Nnauye alitengua uteuzi huo jana alipofanya ziara katika ofisi za BMT kuona miundo mbinu ya ofisi hizo na kujua changamoto zinazowakabili.

“Baraza likirekebishwa vyama vya michezo navyo vinatekeleza majukumu yao na kuleta chachu na maendeleo katika michezo,”alisema Nnauye.

Pia alisema miaka saba ambayo Lihaya amekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza imetosha kwani hakuna mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika sekta ya michezo tangu alipoteuliwa mwaka 2009.

Kutokana na utenguzi huo Nnauye amemtaka Mwenyekiti wa BMT Dionis Malinzi kupendekeza jina la Katibu Mtendaji mpya wa BMT kwa mujibu wa sheria ya BMT kifungu cha 5(1).

Vilevile Nnauye amemtaka Malinzi kuteua Katibu Mtendaji ambaye atakuwa ni mchapa kazi na mwenye mipango ambayo itaibadilisha BMT na kuleta chachu katika michezo nchini.

Nnauye amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara ya habari, utamaduni Sanaa na Michezo kumpangia Lihaya kazi nyingine wizarani.

No comments:

Post a Comment