![](http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2015/1219/r37425_1296x729_16-9.jpg&w=904&h=509&scale=crop&site=espnfc)
Kitu kikuu ambacho kitawasaidia sana kutwaa Ubingwa ni kutokana na wao kuwa na Mechi za Ligi pekee tofauti na Wapinzani wao wengine ambao wanakabiliwa na Mashindano ya Makombe mengine kama vile FA CUP, CAPITAL ONE CUP, UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI.
Wakati wengine, wakati mwingine, wakicheza Mechi 2 au 3 kwa Wiki, Leicester wao watacheza Mechi 1 tu kwa Wiki.
![](http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2016/0209/r52098_1296x729_16-9.jpg&w=738&site=espnfc)
![](http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2016/0209/r52094_2_1296x729_16-9.jpg&w=738&site=espnfc)
Sentafowadi wao Jamie Vardy ndie mashine yao ya Magoli Siku zote akiwa tayari kupokea Pasi ndefu toka nyuma na kuchanja mbuga kwenda Golini kufunga.
Yupo Winga wao Riyad Mahrez, kutoka Algeria, ambae hucheza Kulia na kuingia ndani na kutia Pasi kwa Mguu wake hatari wa Kushoto na pia kuifungia Magoli.
![](http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/media/motion/ESPNi/2016/0207/int_160207_INET_FC_Man_City_v_Leicester/int_160207_INET_FC_Man_City_v_Leicester.jpg&w=738&site=espnfc)
![](http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/media/motion/ESPNi/2016/0208/int_160208_INET_FC_RANIERI_DISC/int_160208_INET_FC_RANIERI_DISC.jpg&w=738&site=espnfc)
Mechi inayofuata kwa Leicester City ni Jumamosi Ugenini na Arsenal ambayo iko Nafasi ya 3 ikiwa Pointi 5 nyuma ya Vinara hao.
Katika Mechi ya kwanza huko King Power Stadium, Arsenal iliichapa Leicester Bao 5-2.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumamosi 13 Februari 2016
15:45 Sunderland v Man United
[Mechi kuanza Saa 12 Jioni]
Arsenal v Leicester
Bournemouth v Stoke
Crystal Palace v Watford
Everton v West Brom
Norwich v West Ham
Swansea v Southampton
Chelsea v Newcastle
Jumapili 14 Februari 2016
16:30 Aston Villa v Liverpool
19:00 Man City v Tottenham
No comments:
Post a Comment