Habari nzito zimevuja kuwa Manchester United imefanya mazungumzo na Wawakilishi wa Jose Mourinho na kwamba imeshakubalika kuwa ataanza kazi rasmi kama Meneja hapo Julai 1.
Meneja wa sasa, Louis van Gaal ana Mkataba na Man United hadi mwishoni mwa Msimu wa 2016/17 lakini hivi sasa mapenzi yake kwa Mashabiki wa Klabu hiyo yametoweka kutokana na Soka bovu na kutokuwa na mtiririko mzuri wa ushindi.
![](http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2016/0205/r50995_1296x729_16-9.jpg&w=904&h=509&scale=crop&site=espnfc)
![](http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2016/1228/r39764_1296x729_16-9.jpg&w=628&h=417&scale=crop&site=espnfc)
Kutokana na uhusiano mzuri kati ya Woodward na Mendes, ambae pia aliwawakilisha Angel di Maria na Radamel Falcao waliotua Old Trafford Msimu uliopita na pia kumwakilisha Kipa David de Gea aliesaini Mkataba mpya na Man United Mwezi Septemba wa Miaka 4, zipo kila dalili kuwa Mourinho ndie atakuwa Meneja anaefuata wa Man United.
No comments:
Post a Comment